Ujumbe wa wafanyabiashara zaidi ya 70 kutoka Tanzania ulioambatana na Rais Samia Suluhu Hassan katika ziara ya kitaifa nchini Urusi unatarajia kutumia jukwaa la uchumi litakalofanyika katika mji wa St. Petersburg kutangaza fursa mbalimbali za biashara zinazopatikana nchini, pamoja na kupata elimu kuhusu mbinu bora za kufanya biashara kutoka kwa wadau mbalimbali watakaoshiriki mkutano huo.

Mhariri Mtendaji wa Idara ya Habari na Matukio Azam TV, Hassan Mhelela, amesema jukwaa hilo ni fursa muhimu ya kukuza mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na Urusi, sambamba na kuwajengea uwezo wafanyabiashara wa Tanzania kuhusu mazingira ya biashara katika masoko ya kimataifa.

Aidha, Mhelela ameongeza kuwa kutokana na vita vinavyoendelea nchini Urusi, uzalishaji wa mbolea umepungua, hivyo kuna ongezeko la mahitaji ya bidhaa hiyo katika soko la Urusi. Amesema hali hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuangalia uwezekano wa kushiriki katika biashara ya mbolea inayohitajika kwa kiwango kikubwa kwa sasa nchini humo.

✍ Ibrahim Kilumbo
Mhariri | John Mbalamwezi
@goodluckpaul_mc
@balqis_njuki
#AzamTVupdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *