Uhaba wa madaktari bingwa katika magonjwa ya mfumo wa chakula na ini kwa watoto umeendelea kuwa changamoto kubwa katika sekta ya afya, hali inayowafanya wataalamu kuendelea kuweka mikakati ya kuwajengea uwezo wahudumu wa afya ili kuboresha huduma na kupunguza athari kwa watoto wanaohitaji matibabu ya kibingwa.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini kwa Watoto, Dkt. Livin Mumburi, amesema baada ya kuhitimu mafunzo maalum ya uzamivu wa kimatibabu nchini Afrika Kusini katika Chuo Kikuu cha Cape Town, ataendelea kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo madaktari pamoja na wanafunzi wa udaktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Dkt. Mumburi amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa na kuwafikia wataalamu wengi zaidi nchini ili kuboresha huduma za kibingwa kwa watoto na kuimarisha mfumo wa tiba katika sekta ya afya kwa ujumla.

Ameongeza kuwa juhudi hizo zitasaidia kuhakikisha changamoto za kiafya zinazowakumba watoto zinapatiwa suluhisho la haraka na sahihi, hatua itakayosaidia kupunguza vifo vinavyotokana na ukosefu wa matibabu stahiki na kuongeza ubora wa huduma za afya nchini.

✍ Ibrahim Kilumbo
Mhariri | John Mbalamwezi
@goodluckpaul_mc
@balqis_njuki
#AzamTVupdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *