
Rais wa Marekani Donald Trump amesema siku ya Jumatano kwamba angependa kukutana na Kiongozi Mkuu wa Iran, Mojtaba Khamenei, akisema katika mahojiano na Gazeti la New York Post kwamba Kiongozi Mkuu wa Iran alihusika katika maamuzi ya Tehran.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Ningependa kukutana naye. Ningependa kukutana na viongozi wote wa Iran, na pengine tutakutana, kulingana na kitakachotokea,” alisema mnamo siku ya Jumatano Juni 3 katika mahojiano na tovuti ya Gazeti la New York Post.
Wairan “wanamheshimu sana,” rais Donald Trump aliongeza. Kiongozi huyo mpya bado hajaonekana hadharani nchini Iran tangu kuteuliwa kwake baada ya kifo cha baba yake katika mashambulizi ya anga yaloyotekelezwa na Marekani na Israel mwishoni mwa mwezi Februari.
Siku ya Jumanne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alisema kwamba Marekani imemwona Mojtaba Khamenei kuwayuko “hai” na “anazidi kushiriki” katika kuongoza Jamhuri ya Kiislamu.
“Kuna dalili kwamba anazidi kujihusisha katika kiwango fulani, ingawa mawasiliano yake yote yamekuwa ya maandishi na kupitia wahusika wengine,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, aliambia Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Bunge la Seneti, akisisitiza ugumu wa kufikisha ujumbe ndani ya serikali ya Iran.
Katika mahojiano yake, Donald Trump pia alibainisha kwamba alijadiliana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusu mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon, ambayo yanatishia makubaliano ya usitishaji mapigano Mashariki ya Kati.
“Ninasumbuliwa kidogo na mapigano yanayoendelea kati ya Isreal na Lebanon. Wakati mmoja, nilisema, ‘Bibi (Benjamin Netanyahu), tunapaswa kuitisha mapigano haya,” Donald Trump alisema.