Nchini Guinea, uteuzi wa maafisa kadhaa katika nafasi mbalimbali unawasilishwa kama kupandishwa cheo, lakini ambalo pia linaweza kutafsiriwa kama kuwaweka mbali baadhi ya maafisa na siasa ya nchi: miongoni mwa maafisa waliobadilishiwa wadhifa ni Waziri wa Ulinzi Aboubacar Sidiki Camara, ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa Guinea nchini Ufaransa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Guinea nchini Ufaransa Paris: nafasi ambayo labda ina hadhi machoni pa baadhi ya watu, lakini ambayo wengine huko Conakry wanaichambua kama aibu kwa mtu ambaye hadi sasa alikuwa Waziri wa Ulinzi.

“Kupandishwa cheo” huku kwa Waziri wa zamani wa ulinzi Aboubacar Sidiki Camara kunaweza kuwa ni matokeo ya mvutano mkubwa zaidi kati yake na mlinzi wake wa zamani: rais wa sasa, Mamadi Doumbouya.

Kwa kweli Aboubacar Camara ndiye ambaye, mnamo mwaka 2012, alimsifu mwanajeshi kijana wa jeshi la Ufaransa kuwa karibu na rais wa Guinea wa wakati huo, Alpha Condé. Matokeo yake, Doumbouya aliteuliwa haraka kuwa mkuu wa vikosi maalum.

Aboubacar Sidiki Camara tayari alikuwa nguzo ya utawala wa Alpha Condé. Naibu mkuu wa jeshi na kisha Mkurugenzi katika ofisi ya Waziri wa Ulinzi, hata hivyo aliteuliwa kuwa balozi wa Cuba na rais wa zamani wa Guinea mnamo mwaka 2019. Baada ya mapinduzi ya Septemba 5, 2021, Aboubacar Sidiki Camara alirudi Conakry. Kisha akateuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi mnamo Oktoba 21.

Waziri wa Usalama ateuliwa kuwa balozi wa Guinea nchini Côte d’Ivoire

Miaka kumi na minne baadaye, mrithi wa Alpha Condé hana imani tena na mshauri wake: tuhuma kuhusu ununuzi wa vifaa vya kijeshi, mikutano ya siri na maafisa wa jeshi wakati mkuu wa nchi alikuwa ziarani nje ya nchi…

Baadhi ya waangalizi wa Guinea wanabaini kwamba tuhuma zinazoendelea kati ya watu hao wawili ni nyingi, hivyo basi rais ameamua kumuweka mbali naye mshirika wake, na hivyo mshirika mwingine wa karibu wa Aboubacar Sidiki Camara, Waziri wa Usalama, Jenerali Bachir Diallo, ameteuliwa kuwa balozi wa Guinea nchini Côte d’Ivoire.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *