Chanzo cha picha, AFP VIA Getty
Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani katika Mashariki ya Kati (CENTCOM) imedai kuwa imedungua ndege mbili zisizo na rubani ambazo ilisema zilirushwa na Iran.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, CENTCOM ilisema:
“Vikosi vya Marekani katika Mashariki ya Kati vilidungua ndege mbili za mashambulizi zisizo na rubani za Iran ambazo zilikuwa zikitishia usafirishaji wa kimataifa katika Mlango wa Hormuz.”
Taarifa hiyo iliongeza kuwa vikosi vya Marekani vinaendelea kubaki katika maeneo yao ya operesheni na viko tayari kuendelea kujilinda dhidi ya kile ilichokitaja kuwa uchokozi wa Iran.
Pia unaweza kusoma: