Machafuko ya kisiasa yaliyotokea jijini Mogadishu nchini Somalia wiki iliyopita, yalisababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi wengine 55, kwa mujibu wa ripoti za serikali.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya imethibitisha taarifa hizo, baada ya kupokea ripoti kutoka hospital mbalimbali jijini Mogadishu.

Makabiliano makali yalizuka kati ya vikosi vya serikali na vile vya upinzani, kuhusu hatua ya kuongezewa muda wa mwaka mmoja kuendelea kuwa madarekani kwa rais Hassan Sheikh Mohamud.

Maandamano ya kupinga kuongeza muhula wa Rais wa Somalia.
Maandamano ya kupinga kuongeza muhula wa Rais wa Somalia. REUTERS – Feisal Omar

Wapinzani wa rais huyo ambaye muda wake ulikuwa umemalizika kuanzia tarehe 15 mwezi Mei, walijitokeza kuandamana Alhamisi iliyopita kushinikiza kufanyika kwa uchaguzi wa urais, wakati machafuko hayo yalipozuka.

Mwezi Machi, wabunge wanaomuunga mkono rais Mohamud, walibadilisha katiba kwa lengo la kuwapa nafasi raia wa kawaida kumchagua kiongozi wa nchi hiyo, na kuondoka na mfuko wa wakuu wa koo kuhusika na zoezi hilo, mpango ambao wapinzani wanasema ni mbinu za kiongozi wa sasa kuendelea kusalia madarakani na kujilimbizia mamlaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *