Jumla ya ndoa 130 zimefungwa kwa pamoja jijini Dar es Salaam katika ibada iliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikma, tukio linalolenga kuimarisha maadili na taasisi ya familia.
Akizungumza baada ya ibada hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobass Katambi, amesema msingi wa maadili unaanzia katika familia, akipongeza taasisi hiyo kwa kuratibu zoezi hilo.
Amesema ndoa halali ni msingi wa kujenga familia imara na jamii yenye maadili, akiongeza kuwa changamoto nyingi za kijamii zinachangiwa na mahusiano yasiyo rasmi na migogoro ya kifamilia.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)