Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imemsimamisha kazi Mwendesha Mashtaka Mkuu, Karim Khan, kwa madai ya utovu wa nidhamu wa kingono na msaidizi wake.

Ofisi ya Baraza la Nchi Wanachama ya ICC yenye wanachama 21, ilitangaza uamuzi huo jana Jumatatu na kusema itawasilisha kesi hiyo kwenye kikao maalumu cha nchi wanachama wa mahakama hiyo.

Ofisi hiyo imesisitiza kwamba kusimamishwa kazi Karim Khan si ishara ya matokeo ya mwisho.

Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa umepata ushahidi kwamba Khan “alifanya ngono bila ridhaa na msaidizi wake” mara kadhaa. Lakini mwezi Aprili jopo la majaji watatu liliamua kwamba uchunguzi huo haukuwa wa mwisho.

Khan alichukua likizo mwaka jana ili kupambana na madai hayo. Raia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 56 amekana mara kwa mara madai hayo.

Madai dhidi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Junai (ICC) yaliripotiwa kwa mara ya kwanza kwa jopo huru la mahakama zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Karim Khan aligonga vichwa vya habari duniani alipofanikiwa kuomba hati za kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na waziri wa zamani wa ulinzi, Yoav Gallant kwa tuhuma za kuhusika na jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu katika vita vya Gaza.

Baadhi wanahusisha kesi hii na msimamo wa Khan wa kuwafuatilia viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *