
Nchini Kenya, polisi wamekabiliana na waandamanaji wanaopinga kujengwa kwa kituo cha karantini cha wagonjwa wa Ebola raia wa Marekani katika Mji wa Laikipia.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kituo hicho ambacho kinajengwa katika kambi ya wanajeshi ya Nanyuki kwenye Mji wa Laikipia, kinatarajiwa kuwahudumia raia wa Marekani wanaoishi nchini DRC ambao huenda wakaambukizwa Ebola.
DRC na Uganda, nchi jirani na Kenya kwa sasa zinaendelea kukabiliana na mlipuko wa virusi vipya hatari vya Ebola.
Kenya haijaripoti kisa chochote cha Ebola na sehemu kubwa ya raia wake wanapinga makubaliano ya Nairobi na Washington ya kujenga kituo cha Ebola katika ardhi yao.
Waandamanaji hao walikusanyika nje ya kambi ya wanajeshi wa angani kwenye Mji wa Laikipia wakiwa wamevalia mavazi maalum yanaotumika hosipitalini, wakibeba majenza yaliokuwa yameandikwa “Ebola”.
Polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji hao, baadhi yao wakikamatwa.
“Hakuna Ebola katika nchi yetu, wanatuletea ugonjwa nchini mwetu,” alisema Zipporah Wachira, 30.
“Ningetaka kufahamu sababu waliona nchi yetu kama eneo la kutupa taka,” alisema Priscilla Waimani, 47, akiwa amejifunga bendera ya Kenya.
Kituo hicho kinatarajiwa kuwa na vitanda 50 vya kuwatenga wagonjwa wa Ebola na kitasimamiwa na maofisa wa afya kutoka nchini Marekani.
Maandamano mengine yalifanyika Juni mosi kupinga ujenzi wake ambapo watu wawili waliripotiwa kuuawa.
Ujenzi wa kituo hicho unaripotiwa kuendelea licha ya agizo la mahakama kuu kutaka usitishwe kwa muda, viongozi wa kisiasa kwenye eneo hilo wakipinga ujenzi huo.
Rais wa Kenya William Ruto ametetea ujenzi huo akisema Marekani imekuwa mshirika muhimu wa nchi yake kwa kipindi cha miaka 25 hadi 30