
Michuano ya soka kuwania kombe la dunia, inaanza leo nchini Marekani, Mexico na Canada.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Sherehe za ufunguzi wa michuano hii mikubwa itafanyika kwa wakati mmoja katika miji itakayoandaa mashindano hayo, yanayoanza leo.
Mechi ya kwanza, itakuwa kati ya Mexico na Afrika Kusini, kuanzia saa nne usiku saa za Afrika Mashariki.
Timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni miongoni mwa mataifa 10 yanayowakilisha bara la Afrika katika mashindano haya.
Kocha wa DRC Sébastien Desabre, anasema vijana wa Leopard wamejiandaa vizuri.
“Tunaenda kuhakikisha kuwa tunafanya vizuri katika michuano hii, wachezaji wametiwa moyo sana, wameahidi kupambana sana. Hatuna lingine, bali kufanya bidii. Tunalenga kufika katika hatua ya 32 bora.” amesema kocha wa DRC.
Mbali na DRC mataifa mengine ya Afrika yanayoshiriki kwenye michuano hii ni pamoja na Morocco, Senegal, Algeria, Tunisia, Misri, Ivory Coast, Ghana, Cape Verde na Afrika Kusini.
Kombe la dunia, linarejea tena nchini Marekani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994, huku Mexico ikiwa mwenyeji baada ya kuandaa michuano hii mwaka 1970 na 1986.
Hata hivyo, Canada inaanda michuano hii kwa mara ya kwanza.
Mechi 104 zitachezwa kwenye miji 16 katika nchi hizo tatu za Amerika Kaskazni, huku mechi ya fainali ikitarajiwa kuchezwa Julai 19 jijini New York.
Kwa mara ya kwanza, timu zitakazoshiriki zimeongezeka kutoka 32 hadi 48.