Mamia ya waandamanaji dhidi ya uhamiaji haramu wameandamana Jumatatu, Juni 8, katika mji mmoja karibu na Johannesburg, Afrika Kusini, siku moja baada ya Rais Cyril Ramaphosa kuahidi kuchukua hatua dhidi ya makundi yanayochochea vurugu za chuki dhidi ya wageni nchini humo.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Maandamano dhidi ya wahamiaji yanaongezeka nchini Afrika Kusini: mamia kadhaa ya waandamanaji walikusanyika siku ya Jumatatu, Juni 8, katika vitongoji vya Johannesburg. Mikusabyiko pia ilifanyika katika majimbo ya Western Cape na Limpopo kudai hatua kali za serikali dhidi ya uhamiaji haramu, ni wakati rais Cyril Ramaphosa alitangaza mfululizo wa hatua siku ya Jumapili jioni kupambana na wahamiaji hawa wasio na hati.

“Matangazo haya yanatia moyo”

Rais Cyril Ramaphosa alitangaza waziwazi kuundwa kwa mahakama maalum ili kuharakisha kufukuzwa kwa wahamiaji wasio na vibali, pamoja na kuimarishwa kwa vikwazo dhidi ya waajiri wanaokiuka sheria ya uhamiaji. Pia aliwaonya wale wanaochochea hasira na vurugu kwa kushambulia biashara ndogo ndogo zinazoendeshwa na wahamiaji wenye hadhi ya kisheria.

“Matangazo haya yanatia moyo,” anaelezea Amir Sheik, mfanyabiashara wa Somalia: “Kilichotutia wasiwasi zaidi ni ukimya wa mamlaka ya Afrika Kusini. Lakini matangazo haya yanatia moyo, hasa wakati rais anasema wazi kwamba polisi na mamlaka ya uhamiaji pekee ndizo zenye haki ya kumkamata mtu. Kwa sababu, hadi sasa, tumeona raia, wamepangwa katika vikosi vya wanamgambo, wakiwanyanyasa wamiliki wa biashara ndogo, wakidai kufungwa kwa maduka yao. Wamiliki hawa wa biashara wana hadhi ya kisheria, hulipa kodi, na huchangia katika uchumi wa taifa.” 

“Rais anaswa pande mbili”

Wakati mvutano ukiongezeka nchini na maandamano yakiongezeka, mkuu wa nchi anajikuta amenaswa pande mbili. Kwa upande mmoja, kuna maoni ya umma yanayopendelea udhibiti mkali wa uhamiaji na kuunga mkono maandamano haya ya kupinga wahamiaji, miezi mitano kabla ya uchaguzi. Kwa upande mwingine, kuna wajibu wa kuheshimu sheria na kuwalinda wageni wenye hadhi ya kisheria. Hii inakuja huku nchi kadhaa zikionyesha hasira zao kwa kile wanachokiona kuwa kutochukua hatua, au hata kutojali, kwa mamlaka ya Afrika Kusini, na zimeanza kuwarudisha raia wao, kama Ghana, Msumbiji, na Zambia.

Afrika Kusini imepitia matukio ya mara kwa mara ya vurugu za kupinga wahamiaji, lakini maandamano yameongezeka mwaka huu, huku wanamgambo wanaojitangaza wakiwaamuru wageni wasio na hati kuondoka nchini ifikapo Juni 30.

“Afrika Kusini ina uchumi mkubwa zaidi barani Afrika na ina zaidi ya wageni milioni tatu, wanaowakilisha zaidi ya 5% ya idadi ya watu wake. Hata hivyo, ukosefu wa ajira unazidi 30%, na kuchochea hasira dhidi ya wafanyakazi wahamiaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *