Wakati walinzi wa pwani wa Mauritania wakiripoti ongezeko kubwa la watu wanaojaribu kuvuka hadi Visiwa vya Canary tangu mwisho wa mwezi Mei, boti zilizozuiliwa ziliondoka kutoka nchi zilizo mbali zaidi kusini, kama vile Guinea na Gambia. Safari hizi zinazidisha hatari kwa wahamiaji wanaotaka kufikia visiwa vya Uhispania.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wahamiaji haramu 1,000 waliookolewa katika pwani ya Mauritania katika siku kumi zilizopita: nchini Mauritania, walinzi wa pwani wanaripoti kuibuka tena kwa wimbi kubwa la wahamiaji katika njia hii hatari ya Atlantiki wanaoondoka kutoka pwani za Afrika Magharibi hadi Visiwa vya Canary vya Uhispania.

Kwa usahihi zaidi, “[wahamiaji] 1,187 wameokolewa tangu Mei 28, 2026, ikiwakilisha umakinifu mkuu wa shughuli za uokoaji katika kipindi hiki cha hivi karibuni,” Ahmed Moulaye, mkurugenzi kitngo kikosi cha walinzi wa pwani wa Mauritania dhidi ya uhamiaji haramu, ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne, Juni 9. Takwimu hii inafikisha idadi ya wahamiaji waliookolewa na mamlaka hadi 1,417 tangu mwanzo wa mwaka.

Safari hizi hatari zilianza tena mwishoni mwa mwezi Mei, siku chache baada ya sikukuu ya Tabaski (Eid al-Adha), kwa kasi ambayo ni ishara mbaya kwa Ahmed Moulaye, ambaye anabaini kwamba ikiwa itaendelea, “wahamiaji wanaweza kufikia kiwango kisicho cha kawaida mwaka huu,” ingawa, kwa sasa, hakujawa na waliofika katika Visiwa vya Canary, na kwa hivyo hawajaweza kufanikiwa kuvuka sehemu yoyote. Miongoni mwa boti zilizozuiliwa, nane zilitoka Gambia na Senegal.

Ukaguzi umeongezeka

Wote waliookolewa wamepelekwa kwenye vituo vya muda vya mapokezi kwa wageni vinavyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya, vilivyoko Nouakchott na Nouadhibou. Vituo hivi ambavyo vimeekwa kutathmini ustahiki wao kwa ulinzi wa kimataifa, vinawahudumia manusura kwa muda usiozidi saa 72, muda unaohitajika “kuamua hali yao binafsi.”

Tangu makubaliano yaliposainiwa kati ya nchi za Ulaya na baadhi ya nchi za Afrika kwenye pwani ya Atlantiki, kama vile Moroco na Mauritania, udhibiti umeongezeka ili kuzuia vivuko vya kwenda Ulaya, jambo ambalo kwa kiasi fulani linaelezea ongezeko la idadi ya uokoaji iliyorekodiwa. Matokeo mengine ni safari za wahamiaji, ambapo watu wanazidi kuondoka kutoka kusini zaidi, kutoka Gambia au Guinea, hivyo kuongeza muda wa vivuko na hivyo kuongeza hatari za kupotea baharini au kuzama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *