Matangazo ya kibiashara

Asubuhi ya tarehe 7 Februari, 2025, mwandishi wa habari wa gazeti la mtandaoni la Pinnacle News Arlindo Chissale, aliondoka nyumbani kwake Pemba, mji mkuu wa mkoa wa Cabo Delgado eneo la kaskazini mwa Msumbiji. Alikutana na rafiki yake, Abudo Gafuro, mbele ya kanisa la Maria Auxiliadora.

Mwandishi wa habari alikuwa akirekodi video ambapo alizungumzia udanganyifu wa uchaguzi. Kwa miezi kadhaa, nchi ilikuwa imetikiswa na maandamano kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba. “Nitaichapisha usiku wa leo,” aliahidi, huku wanaume hao wawili wakitengana.

Saa chache baadaye, Arlindo Chissale alichukua basi la kwenda Nacala, kilomita kama mia chache kusini. Alitakiwa kwenda kazi yake ya pili, kwenye makaburi jijini. Chissale hakufika kamwe. Miezi kumi na saba baada ya kutoweka kwake, bado hajulikani alipo.

Vitisho

Saa za mwisho za kuonekana kwa Arlindo Chissale zinasimuliwa na kaka yake, Macario. Kwa mujibu wa mashahidi aliokutana nao, basi alilotumia mwandishi huyu wa habari lilisimamishwa karibu na kijiji cha Silva Macua, yapata kilomita 100 magharibi mwa Pemba, na gari jeupe lisilokuwa na alama yoyote. Wanaume watano walitoka kwenye Gari hilo,  wawili kati yao wakiwa wamevaa sare za polisi. Walimlazimisha mwandishi huyo atoke nje, wakampiga, kisha wakamsukuma ndani ya gari.

Kutoweka kwa Arlindo Chissale hakukuwashangaza wale walio karibu naye. “Alikuwa ametuandaa kwa mabaya zaidi,” kaka yake alikiri. “Hivi majuzi, alihisi kutishiwa na kuteswa.” Kwa miaka kadhaa, mwandishi huyo alikuwa akifanya kazi kwenye mada nyeti: ugaidi unaotikisa eneo hilo, unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na Jeshi la Msumbiji (FADM), ufisadi, na biashara ya dawa za kulevya.

Kabla tu ya kutoweka, mwandishi huyo aliitwa usiku sana kwenye kituo cha mafuta na Bernardo Ouana, kamanda wa kituo cha 3 cha polisi huko Pemba. Mkutano ambao ulizua wasiwasi kwa familia yake na marafiki zake.

Mauaji yaliyotekelezwa na wanajihadi nchini Msumbiji
Mauaji yaliyotekelezwa na wanajihadi nchini Msumbiji © Baptiste Condominas

Ukandamizaji wa Vyombo vya Habari

Haki iliyompata Arlindo Chissale sio tukio la kipekee huko Cabo Delgado. Mnamo mwaka wa 2020, mwanahabari wa kituo cha redio ya jamii huko Palma kaskazini mwa Pemba, Ibraimo Abù Mbaruco, alitoweka katika mazingira yenye kutatanisha katika hali kama na hiyo. Kulingana na taarifa kutoka Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA), maneno yake ya mwisho yalitumwa kwa ujumbe mfupi kwa mwenzake: “Nimezungukwa na wanajeshi.”

Mwaka mmoja kabla, mwandishi wa habari Amade Aboubacar alifungwa gerezani kwa Muda wa miezi minne kizuizini kabla ya kesi baada ya kukamatwa alipokuwa akiwahoji watu waliokimbia makazi yao kufuatia mashambulizi ya kundi la al-Shabaab.

Akituhumiwa kwa “uchochezi wa umma” na “kuwatukana mamlaka ya umma,” Amade Aboubacar hatimaye aliachiliwa kwa dhamana. Mashtaka hayo yalifutwa tangu wakati huo. “Watu walioko huko wanateswa na vikosi vya serikali,” anaelezea Vasco King wa shirika la haki za binadamu la Kundeleya.

Sheria ya Ukimya

Cabo Delgado inapatikana kwenye umbali wa kilomita takribani 3,000 kutoka mji mkuu wa Msumbiji, Maputo. Mkoa huu, wenye utajiri wa malighafi (kama rubi, lithiamu, ardhi adimu, na gesi), ni Mkoa ambao umebaki kuwa maskini zaidi nchini.

Eneo hilo pia ni eneo la shughuli nyingi haramu: dawa za kulevya, pembe za ndovu, wanyama wa kitropiki, na mbao, ni Shughuli ambazo hustawi kutokana na kutokuwepo kwa mamlaka ya serikali kwa kiasi kikubwa. Kwa karibu miaka 10, jimbo hilo pia limekumbwa na vurugu kutoka kwa kundi la Kiislamu lenye silaha, al-Shabaab.

Soma pia:https://www.rfi.fr/sw/afrika/20260609-msumbiji-unyang-anyi-wa-maliasili-unachochea-ugaidi-wa-al-shabaab

Tarehe 17 mwezi wa Februari 2024, wakati wa hotuba huko Pemba, gavana wa Cabo Delgado, Valige Tauabo, hakusema maneno mengi. Kulingana naye, habari za vyombo vya habari kuhusu eneo hilo “zina alama ya maovu tu yanayofanyika.” Alishutumu vyombo vya habari kwa kufanya “mikataba na magaidi.”

Serikali ya Msumbiji haitaki sura halisi ya mgogoro ifichuliwe,” anaelezea Carlos Qembo, mtafiti wa Shirika la Amnesty International. “Hapo awali, mamlaka ziliamini kwamba vurugu huko Cabo Delgado zilikuwa matokeo ya ushawishi wa nje na zingetatuliwa haraka. Licha ya rasilimali zake nyingi za madini, Cabo Delgado inakabiliwa na ukosefu mkubwa wa usawa wa kijamii, huku vijana wakiwa ndio waathiriwa wakubwa. Mamlaka hayataki tafsiri hii ya hali hiyo ijulikane na wote na kuendelea.”

Mfumo huu wa uchambuzi wa jinsi mambo yalivyo unatia wasiwasi zaidi ikizingatiwa kwamba kuibuka kwa al-Shabaab kulitokea muda mfupi baada ya ugunduzi wa uwanja mkubwa wa gesi duniani mwaka wa 2012: mita za ujazo bilioni 5, zinazotarajiwa kuvutia wawekezaji wa kimataifa.

Magari yaliyoharibiwa katika mji wa Mocimboa da Praia mkoani Cabo Delgado
Magari yaliyoharibiwa katika mji wa Mocimboa da Praia mkoani Cabo Delgado © Baptiste Condominas

Sera ya Mbuni

Mamlaka Kukataa kuzichambua sababu za mgogoro huo kumezua mfumo wa ukandamizaji, na hii ni kwa mujibu wa mratibu wa Kituo cha Demokrasia na Haki za Binadamu (CDD) Bwana Aly Caetano. “Mwanaharakati anaposhutumu ukosefu wa ajira au umaskini, anashutumiwa kuwa adui wa nchi,” anaelezea.

Mwanya Huu ambao Al-Shabaab wameutumia vibaya. Katika mahubiri na propaganda zao, magaidi hawa wanalaani matumizi mabaya ya utajiri, ufisadi, na ukosefu wa usawa wa kijamii, huku mamlaka zikipitisha sera kali ya ukandamizaji dhidi ya raia wa kawaida.

Serikali ilichukua muda mrefu kutangaza hali ya dharura,” anaongeza kusema Aly Caetano. “Hata hivyo, ilizuia haraka uhuru wa wakazi wa Cabo Delgado. Katika Palma na Mocimboa da Praia, haki za kutembea na kujumuika zimepunguzwa.” Mwanaharakati huyo hata anataja hofu ambayo baadhi ya watu wanayo ya kufuata dini ya Kiislamu.

Mnamo mwaka wa 2023, serikali ilipunguza zaidi uhuru wa raia. Kwa kisingizio cha kupambana na utakatishaji fedha, muswada wa sheria ulianzishwa ambao ungeruhusu kufutwa kwa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali, NGOs na mashirika ya haki za binadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *