.

Chanzo cha picha, US Navy via Getty Images

Kituo kikuu cha kuendesha oparesheni za kijeshi Marekani (CENTCOM) imedai kuwa vikosi vyake vimeangusha ndege kadhaa zisizo na rubani zilizorushwa na Iran kuelekea Mlango bahari wa Hormuz.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, CENTCOM ilisema Iran ilirusha ndege zisizo na rubani kadhaa kwa lengo la kulenga meli za kibiashara zilizokuwa zikisafiri kupitia Mlango bahari wa Hormuz.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, “Vikosi vya Marekani vimedungua ndege hizo zote zisizo na rubani katika saa chache zilizopita, na usafiri wa meli kupitia Mlango wa Hormuz unaendelea bila usumbufu wowote.”

Centcom ilisema ndege hizo za Iran zilikuwa tishio kwa usalama wa meli za kibiashara zinazopitia eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *