Zaidi ya washiriki 3,000 wanatarajiwa kushiriki jukwaa la mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) litakalofanyika Oktoba 20 hadi 22 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma, likijadili namna ya kuimarisha uendelevu wa shughuli za mashirika kwa kupunguza utegemezi wa ufadhili wa nje na kuongeza vyanzo vya ndani vya mapato.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO), Jasper Makala, amesema jukwaa hilo litatoa fursa kwa wadau kubadilishana uzoefu na kujadili mikakati ya kujenga uwezo wa mashirika kujitegemea kifedha na kuendelea kuchangia maendeleo ya taifa.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)