Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Prof. Makame Mbarawa, ametoa maelekezo kwa taasisi za sekta ya usafiri wa anga nchini kuhakikisha Uwanja wa Ndege wa Shinyanga unakamilika kwa wakati ili kuanza kutoa huduma za usafiri wa anga kuanzia Septemba 1, 2026.
Maelekezo hayo yametolewa wakati wa zoezi la majaribio ya kutua na kuruka ndege katika Uwanja wa Ndege wa Shinyanga, ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali na wadau wa sekta ya usafiri wa anga walishiriki tukio hilo mhimu
Prof. Mbarawa amesema ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Shinyanga ni sehemu ya mkakati wa Taifa wa kuimarisha usafiri wa anga nchini. Na kutasaidia kuvutia uwekezaji katika sekta za utalii, biashara na madini, pamoja na kufupisha muda wa usafiri kwa wananchi na wafanyabiashara na kuelekeza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mradi unakamilika kabla au ifikapo Septemba 1, 2026 na kuwataka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kuhakikisha taratibu zote za kiufundi na kisheria zinakamilika kwa wakati kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.
Kwa upande wao wadau wa usafili wa anga mkoa wa Shinyanga wakiwemo wakala wa usafili wa anga BEIBAMAR Travel Agent wamesema kuanza kwa safari za anga kupitia uwanja wa ndege wa Shinyanga kutasaidia kupunguza adha ya wasafiri kutoka Shinyanga na maeneo jirani kusafiri umbali mrefu kufata huduma hiyo katika mkoa jirani wa Mwanza,
#startvupdates
(Feed generated with FetchRSS)