
Baada ya polisi kuzima siku ya Ijumaa mandamano ya upinzani dhidi ya marekebisho ya katiba yaliyopendekezwa ambayo yanahusishwa na kambi ya rais, malalamiko yameongezeka kutoka kambi moja kweda nyingine. Serikali inalaani vurugu zilizotokea siku ya Ijumaa huko Kinshasa, inataja majeraha miongoni mwa waandamanaji na vikosi vya usalama, na kutangaza uchunguzi ili kubaini waliohusika. Wakati huo huo, upinzani unaendelea kuhesabu wanaharakati wake waliokamatwa na kujeruhiwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Pascal Mulegwa
Baada ya makabiliano kati ya vikosi vya usalama na waandaanaji wenye hasira, vyama vya upinzani vinajaribu kuwapata wanaharakati wao waliokamatwa wakati wa maandamano ya siku ya Ijumaa. Viongozi wa kisiasa na wanasheria wametumwa katika vituo kadhaa vya polisi huko Kinshasa. Hata baadhi ya vitengo vya idara ya ujasusi vinaendelea kutafuta waliohusika katika maandamano hayo ambapo, kulingana na makundi ya raia, wanaharakati kadhaa wanadaiwa kuchukuliwa na kupelekwa kusikojulikana.
Kulingana na chanzo cha polisi, idadi kubwa ya waliokamatwa waliachiliwa siku ya Jumamosi jioni. Hata hivyo, wale wanaochukuliwa kuwa waliohusika zaidi katika kuandaa maanamano hayo bado wako kizuizini.
Watu 189 walijeruhiwa vibaya na watu watatu kuteguka kwa viungo
Chama cha Jean-Marc Kabund, Alliance for Change, kinadai kurekodi watu 189 waliojeruhiwa vibaya, watu watatu waliovunjika mikono na miguuu, na wengine kadhaa walikamatwa. Chama hicho kinaishutumu serikali kwa kutumia wanamgambo kushambulia waandamanaji pamoja na polisi.
Katika hospitali, wengi wa wale walio na majeraha madogo waliruhusiwa kuondoka siku ya Ijumaa. Hata hivyo, baadhi ya watu waliojeruhiwa viaya bado wako chini ya uangalizi wa kimatibabu. Mmoja wa wanaharakati walioripotiwa kufariki na upinzani hatimaye alipatikana akiwa hai, lakini akiwa katika hali ya kukosa fahamu, kulingana na ECIDE, chama cha Martin Fayulu.
Serikali inasema inataka kujua chanzo cha vurugu hizi.
Ubelgiji ni nchi ya kwanza ya Magharibi kuzungumzia kuhusu hali hii. Waziri wake wa Mambo ya Nje, Maxime Prévot, amelaani matumizi mabaya ya nguvu, matumizi ya nguvu kupita kiasi, na uporaji wa mali na vitu katika makao makuu ya chama cha siasa, akisema kwamba vitendo hivyo havina nafasi katika demokrasia.