
Idadi ya wagonjwa waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya Ebola nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imeongezeka na kufikia 782, ikiwemo vifo 178n wakati huu mlipuko huo ukienea kwenye maeneo mawili mapya, mamlaka zimethibitisha.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa data zilizotolewa hapo jana na serikali ya DRC maambukizi mapya 72 yalirekodiwa katika muda wa saa 24 na hivyo kuongeza idadi ya wagonjwa wa ebola hadi kufikia 782.
Takwimu zinaonesha kwamba mlipuko huo, ambao ni wa 17 nchini Congo, unabaki katika majimbo matatu mashariki mwa nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.
Katika hatua nyingine wafanyakazi wa afya na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayopambana na janga hili, wamekuwa wakikumbana na uadui kutoka kwa baadhi ya jamii, hali ambayo inaathiri ufuatiliaji na huduma kwa wagonjwa, huku pia imani potofu na kuenea kwa habari za uongo kukihatarisha juhudi zinazoendelea.