#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametoa muda wa mwezi mmoja kwa wamiliki wa gereji na mafundi seremala kuondoa magari na samani chakavu pembezoni mwa barabara ili kurejesha unadhifu wa jiji.

Akizungumza katika kikao kazi maalum kilichokutanisha wakuu wa wilaya, madiwani, na watendaji wa mitaa na kata, Chalamila amesisitiza kuwa vyuma hivyo vinaharibu muonekano wa jiji.

Aidha, amewataka viongozi hao kuimarisha ulinzi kwa kuanzisha vikundi vya sungusungu na kulinda amani kufuatia uvumi wa uwepo wa maandamano, akifafanua kuwa Dar es Salaam ndio kitovu cha uchumi na diplomasia nchini.

Sanjari na hayo, RC Chalamila ameagiza halmashauri zote kuwa na madampo, akitoa hadi Julai 30 kuanza kwa uendeshaji wa dampo la Pugu Kinyamwezi kwa ubia na sekta binafsi, huku akipiga marufuku ubandikaji hovyo wa matangazo na utoaji wa vibali vya baa kwenye maeneo ya makazi kama Masaki na Osterbay.

Amewataka viongozi kusimamia usafi na upakaji rangi majengo ya barabarani kuelekea michuano ya AFCON ili kulinda heshima ya taifa. Katika kikao hicho, Katibu Tawala wa Mkoa, Abdul Mhinte, amesisitiza matumizi ya anwani za makazi ili kurahisisha utambuzi wa watu na kuimarisha usalama.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
‎Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
‎Capitalradio Tanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *