#HABARI: Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakari Zubeir Ally, amemuomba Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, kumshawishi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ili siku ya mapumziko ya Mwaka Mpya wa Kiislamu (Hijriyya) itambuliwe Tanzania nzima.

Mufti Zubeir ametoa ombi hilo leo Juni 15, 2026 wakati wa maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kiislamu visiwani Zanzibar, akieleza kuwa Tanzania ni nchi moja hivyo mapumziko hayo yanapaswa kuwanufaisha Waislamu wa pande zote za Muungano.

Amesema hatua ya Rais Mwinyi kutangaza siku ya mapumziko kwa Zanzibar ni jambo la kupongezwa, huku akionesha matumaini kuwa ushauri huo unaweza kufikishwa kwa Rais Samia ili utaratibu huo uweze kuenea nchi nzima.

Awali, Rais Dkt. Mwinyi alitangaza kuwa Jumatano Juni 17, 2026 itakuwa siku ya mapumziko Zanzibar kwa ajili ya kuadhimisha na kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu 1447 Hijriyya.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *