
Brigedia Jenerali Esmail Qaani, kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), amesema kuwa vita vya tatu vya kulazimishwa dhidi ya Iran vimeifedhehesha kabisa Marekani na vimeharakisha kuporomoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Katika mahojiano ya kina Jumatatu usiku, Kamanda Qaani alisema,Jenerali Qaani amesisitiza kuwa mizizi ya Muqawama au mapambano ya Kiislamu katika eneo ilianza tangu siku za mwanzo za Mapinduzi ya Kiislamu, wakati Imam Khomeini (MA) alipoagiza kuundwa kwa makundi ya Muqawama katika maeneo mbalimbali ya eneo la Asia Magharibi.
Baada yake, Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, aliendeleza njia hiyo kwa uthabiti, na kuyafanya makundi hayo kuwa harakati zenye nguvu zilizokuja kuungana na kuunda mhimili wa Muqawama. Amesema harakati hizo zimeitia hofu Marekani, madola yote ya kiistikbari duniani na utawala wa Kizayuni.
Jenerali Qaani amesema: “Leo, Marekani inafahamu vyema, na utawala wa Kizayuni unafahamu hata zaidi, kwamba nguvu inayosimama imara dhidi yao, katika mazingira magumu zaidi, bila kuondoka uwanjani, ni harakati za Muqawama.”
Kamanda huyo wa Kikosi cha Quds cha IRGC amefichua kuwa makundi ya Muqawama yalikuwa tayari yameamua, muda mrefu kabla ya vita, kusimama mstari wa mbele dhidi ya Marekani ili kulilinda Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Alitaja kwa namna maalum nafasi ya Hizbullah ya Lebanon, amebainisha kuwa harakati hiyo ilipigana bega kwa bega na Iran kwa siku 104.
Amesema: “Hizbullah haiwezi kuvunjwa. Hakuna yeyote anayeweza kusimama dhidi ya Hizbullah ya Lebanon.”
Jenerali Qaani amesema kuwa adui wa Kimarekani na Kizayuni amepoteza hadhi katika kila eneo alipokutana na wapiganaji wa Muqawama.
Amelitaja eneo la Lango-Bahari la Bab al-Mandab kama moja ya karata muhimu za Muqawama na kuongeza kuwa eneo hilo ni ngome muhimu mwa vijana wa Hizbullah, Ansarullah na Yemen kwa ujumla.
Amefichua kuwa baadhi ya meli za kivita za kisasa zaidi za Marekani ambazo zilipanga kuvuka Bahari Nyekundu wakati wa vita dhidi ya Iran zilitumia takriban wiki mbili zikisita kati ya Yemen na Jeddah, na hatimaye zikaogopa kuvuka.