Ghana ni mwenyeji wa mkutano wa siku tatu, kujadili namna mataifa ya Afrika yanavyoweza kupata haki baada ya Umoja wa Mataifa kupitisha azimio, kuwa biashara ya utumwa dhidi ya waafrika, ulikuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kuwahi kutokea.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa nchi na serikali, viongozi wa mashirika ya kiraia, wanahistoria na watafiti, wanakutana jijini Accra kujadili hatua za kuchukua baada ya azimio hilo la Umoja wa Mataifa.

Wajumbe wanaohudhuria mkutano huu, wanajadili masuala matano muhimu, likiwemo namna wanavyoweza kuja na mipango au sera za kupata haki kwa kupata fidia kutoka kwa mataifa yaliyohusika na biashara ya utumwa.

Mkutano huu unakuja miezi mitatu baada ya pendekezo hili la Ghana, kupitishwa na Umoja wa Mataifa, kutambua kuwa biashara ya utumwa kutoka waafrika kwenda katika mabara mengine kutambuliwa kama ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Uingereza na mataifa yote ya Umoja wa Ulaya, yaliyohusika pakubwa katika biashara hiyo hawakupigia kura mswada huo, kupinga utumwa wa Waafrika uliodumu kwa miaka 400 kati ya Karne ya 16 hadi ile ya 19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *