Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akizungumza na raia wa nchi yake wanaoishi Houston, nchini Marekani, amemshtumu bila kumtaja mtangulizi wake, Joseph Kabila kwa kuchochea hali ya kisiasa inayoendelea nchini DRC.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais Tshisekedi, amemshtumu mtangulizi wake bila kumtaja jina na washirika wake ikiwemo nchi Jirani ya Rwanda, kwa kuendelea na harakati zao za kupora rasilimali za nchi hiyo yenye utajiri wa rasilimali ya madini.

Aidha, Tshisekedi amewataka Wakongamani kuungana na kukataa kile alichosema ni maadui wa nchi hiyo, huku akiahidi kuwa jeshi la FARDC litachukua maeneo yote yanayodhibitiwa na waasi wa M23/AFC Mashariki mwa DRC.

Washirika wa karibu wa Kabila, wakiongozwa na mwanasiasa Félix Momat, wamelaani matamshi ya Tshisekedi, wakisema kauli zake zinadunisha nafasi yake na Ofisi ya urais nchini DRC.

Kauli hii ya Tshisekedi, inakuja baada ya Maseneta wiki hii kupitisha mswada muhimu unaoweka msingi wa kubadilisha Katiba, kitendo ambacho wapinzani wanaona kuwa, ni mpango wa kiongozi huyo kutaka kuendelea kusalia madarakani, wakati muhula wake utakapotamatika mwaka 2028.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *