Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge), Mohammad Baqer Qalibaf, ambaye anaongoza timu ya mazungumzo na Marekani, ameeleza kuwa malipo ya kuvuka katika Lango-Bahari la Hormuz yamejumuishwa kwenye Hati ya Makubaliano baina ya pande hizo mbili na kwamba kupita katika lango hilo katika kipindi hiki cha siku 60 cha mazungumzo kutakuwa bure.

Qalibaf pia amezungumzia mada mbalimbali kuhusu vita na mazungumzo ya karibuni katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya taifa.

Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa hali ya Lango Bahari la Hormuz haitarejea katika mazingira ya kabla ya vita.

Amesema Iran ina haki ya mamlaka ya kujitawala katika Lango-Bahari la Hormuz na kupokea fedha za ushuru kwa ajili ya huduma zinazotolewa hapo, na kwamba hii haina maana kuwa Iran ina nia ya kupuuza sheria za kimataifa au sheria za safari za baharini.

Ameendelea kusema kuwa: Iran ina mpango wa kutoza fedha kwa meli zote zitakazovuka lango hilo baada ya kupita bila malipo kwa siku 60.  

Spika wa Bunge la Iran pia amezungumzia athari za vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran kwa uchumi wa dunia akisema: Vita vya karibuni vimekuwa na athari mbaya kwa upande wa kijiografia, kijeshi na kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *