Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3
Zaidi ya siku 100 baada ya Marekani na Israel kuivamia Iran, pande zote mbili zinadai ushindi.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yamekamilika ila mazungumzo magumu zaidi ndiyo yanaanza sasa.
Pande zote mbili zimepigia upato makubaliano hayo na kujiita washindi, lakini kulingana na wachambuzi, hakuna upande ulioshinda kwani hakuna taifa ambalo limefanikiwa kuwashawishi raia wake na upinzani kushabikia mkataba huo, wakosoaji wa kila upande wakisema inanufaisha adui.
Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images
Kwa Iran, makubaliano na Marekani yanatoa ni muhimu kwa usitishaji mapigano, na kudai kuwa wameibuka kutoka kwa mgogoro huu na nguvu zaidi.
Lengo kuu la Tehran katika vita hivi halikuwa lazima kuishinda Marekani na Israel kwa njia ya kijeshi ya moja kwa moja. Badala yake, lilikuwa ni kuhakikisha kwamba Jamhuri ya Kiislamu inabakia imara, uongozi wake ukiendelea kufanya kazi, na nafasi yake ya kufanya mazungumzo pia inasalia imara.
Na kulingana na hati ya makubaliano yaliyoafikiwa, hati hiyo inaonyesha Iran imeafikia lengo hilo, kwani utawala wake hujasambaratika.
Hati hiyo, iliyosainiwa na Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, inatoa muda wa siku 60 wa mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Hata hivyo, pia inaagiza kusitishwa mara moja kwa operesheni za kijeshi pande zote, ikiwemo Lebanon, kuheshimiana kwa mamlaka ya kila nchi, kufunguliwa upya kwa Mlango bahari wa Hormuz, na kuondolewa kwa kizuizi cha majini cha Marekani dhidi ya meli za Iran.
Tehran imekubali kusaidia kuhakikisha usafiri salama wa meli za kibiashara kupitia Mlango bahari wa Hormuz, jambo ambalo kwa muda mrefu kabla ya vita lilikuwa hali ya kawaida pia imesema kwamba haitatengeneza silaha za nyuklia.
Ahadi za Marekani zinaonekana kuwa pana zaidi. Kulingana na makubaliano hayo, Washington itaanza na kuondoa kizuizi chake cha majini, kutoa vikwazo kwa mauzo ya mafuta ya Iran, kuwezesha upatikanaji wa mali za Iran zilizozuiliwa, kulegeza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran, na kwa kushirikiana na washirika wa kikanda kuendeleza mpango wa ujenzi upya na maendeleo ya kiuchumi kwa Iran wenye thamani ya angalau dola bilioni 300 .
Chanzo cha picha, Getty Images
Masuala magumu zaidi yameahirishwa, bila kutatuliwa.
Mustakabali wa urani ya Iran iliyorutubishwa itajadiliwa baadaye.
Hata hivyo, kutoafikia maelewano pia kunaweza kuwa na hatari.
Iwapo Tehran haitasitisha mpango wake wa nyuklia, mchakato mzima wa kupatikana kwa amani unaweza kusambaratika. Hii inaweza kuipa Israel na Marekani kurejea tena katika vita.
Ulinganisho na makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 na sasa hauwezi kuepukika.
Baadhi ya viongozi wa Marekani wanaiona mkataba huo kama mbaya zaidi ikilinganishwa na ule wa Barack Obama ulioafikiwa mwaka wa 2015, kwani hii ya sasa inaipa Iran nafuu zaidi.
Huko Tehran, wale wenye misimamo mikali wanaishtumu serikali kwa kurudia ‘usaliti’ wa 2015.
Iran imepata afueni ila bado haijapata makubaliano ya mwisho nay a kudumu. Siku 60 zijazo zinaweza kubadili taswira ya makubaliano hayo.