
Jeshi la utawala wa Kizayuni limetangaza kuuawa na kujeruhiwa askari wake 22 katika mapigano ya jana Alhamisi jioni na vikosi vya muqawama vya Hizbullah ya Lebanon.
Jeshi la utawala wa Kizayuni limekiri kuwa maafisa na askari wake 17 walijeruhiwa katika mapigano yaliyotokea jana usiku huko kusini mwa Lebanon, ambapo baadhi yao walilazimika kukatwa viungo vya miili. Kwa kuongezea, askari watano, pamoja na kamanda wa kikosi, waliuawa kwa kombora la kulipua vifaru na magari ya kijeshi.
Wakati huo huo, wapiganaji wa Kiislamu wa Lebanon wametangaza kwamba wapiganaji wa Hizbullah, kwa kufanya shambulio kubwa la makombora ya kuongozwa kutokea mbali, waliharibu vifaru vitatu vya Merkava vya jeshi la Israel katika eneo la kimkakati la Ali Taher – Kaftar Benit, na kuibua hamasa kama ya Karbala kwa kuua makumi ya vikosi vya adui.