Kama sehemu ya juhudi za kuwalinda raia na kupambana na makundi yenye silaha, walinda amani wa MONUSCO na vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC) wamefanya operesheni kadhaa za pamoja katika eneo la Irumu katika mkoa wa Ituri tangu mwanzoni mwa wiki hii.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Huko Komanda, doria ya ufuatiliaji ilifanywa kuzunguka kijiji cha Bavonkutu ili kutathmini hali ya usalama na kuwahakikishia wakazi wa eneo hilo.

Kulingana na msemaji wa Jeshi la MONUSCO Kanali Charles Idjiwa, misheni hii ililenga hasa kuzuia vitisho vyovyote vinavyoweza kutokea na kudumisha mazingira salama katika eneo hilo.

“Doria iliyofanywa katika kijiji cha Bavonkutu ililenga kuzuia vitisho vyovyote vinavyoweza kutokea, kuwahakikishia wakazi wa eneo hilo, na kuhakikisha mazingira salama na mazuri kwa shughuli zao za kila siku,” alielezea.

Wakati wa operesheni hii, timu za pamoja zilifanya uchunguzi na tathmini ya hali ya mambo.

“Tathmini zilizofanywa zilithibitisha kwamba eneo hilo linaendelea kuwa shwari na liko chini ya udhibiti, bila dalili zozote za shughuli za makundi yenye silaha au matukio makubwa yaliyoripotiwa,” alisema Kanali Idjiwa.

Wakati huo huo, walinda amani wa Umoja wa Mataifa walioko Tchabi, wakiambatana na FARDC (Vikosi vya jeshi laJamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), walizuru mji wa Kiyangele.

Timu hizo zilikutana na viogozi wa eneo hilo na wakazi kukusanya taarifa kuhusu hali ya usalama na wasiwasi wa wakazi.

Kulingana na MONUSCO, mazungumzo haya yalisaidia kuimarisha uhusiano na jamii za wenyeji huku yakiongeza uelewa miongoni mwa wakazi kuhusu hatua za kuzuia Ebola.

Kuimarisha imani na ulinzi wa raia

Kwa misheni ya Umoja wa Mataifa, shughuli hizi ni sehemu ya mkakati wa kijamii unaolenga kuboresha ulinzi wa raia katika maeneo yaliyoathiriwa na ukosefu wa usalama.

“Misheni hii imeimarisha ushirikiano na uaminifu kati ya MONUSCO na jamii za wenyeji,” alibainisha msemaji wa kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *