jk

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 4

Akili unde imetumika kutengeneza aina ya chanjo mpya ambayo inaweza kukulinda dhidi ya aina mbalimbali ya virusi na kuzuia magonjwa ya mlipuko, kulingana na watafiti.

Timu kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge inasema hii ni mara ya kwanza kwa chanjo kubuniwa na akili unde (AI) moja kwa moja na kisha kufanyiwa majaribio kwa wanadamu.

Chanjo hiyo iliundwa ili kufanya kazi dhidi ya virusi vyote vya korona, ikiwa ni pamoja na aina zote za Covid pamoja na virusi ambavyo kwa sasa vinaambukizwa kutoka kwa wanyama.

Chanjo hiyo bado iko katika hatua zake za awali, lakini timu tayari inatengeneza chanjo nyingine ambazo zinaweza kupambana na mafua na virusi vya Ebola.

Chanjo hufundisha miili yetu jinsi ya kugundua maambukizi ili kuongeza nafasi zetu za kuyapambana nayo.

Lakini baadhi ya virusi vina uwezo wa kubadilisha mwonekano wao, au kubadilika, kwa hivyo chanjo zinaweza kukosa ufanisi. Ndiyo maana chanjo za COVID-19 na mafua ya majira ya baridi zinahitaji kuboreshwa mara kwa mara.

Inafanyaje kazi?

j

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa kawaida, chanjo hutengenezwa kwa kutumia aina ya virusi.

Watafiti wa Cambridge walichukua vinasaba kutoka aina mbalimbali za virusi vya korona. Vinasaba hivi vilichambuliwa kwa kutumia akili unde.

Kisha akili unde ikabuni protini yenye uwezo wa kufunza mfumo wa kinga ili kuulinda dhidi ya aina zote za virusi vya korona, hata kama vinabadilika au kuna maambukizi mapya kutoka kwa wanyama hadi kwa wanadamu.

Majaribio yaliyofanywa kwa watu 39, yalibuniwa kutathmini kama chanjo hizi ni salama. Utafiti wa pili, uliowahusisha takriban watu 200, utatoa uelewa bora wa kiwango ambacho chanjo hiyo hufunza mfumo wa kinga.

Matokeo ya utafiti yameelezwa kwa kina katika Jarida la Infection, yanaonyesha kwamba utendaji kazi wake kwenye mfumo wa kinga ulikuwa “wa kawaida,” lakini bado inaleta matumaini.

Timu ya Cambridge tayari inafanya utafiti kwa wanyama kuhusu chanjo za mafua ya msimu ambazo hazitahitaji kubadilishwa kila mwaka na chanjo dhidi ya mafua ya ndege aina ya H5N1.

Pia wanatafiti chanjo dhidi ya homa ya kutokwa na damu inayosababishwa na virusi, ambayo inajumuisha spishi za Ebola.

Mlipuko wa sasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unasababishwa na spishi ambayo hakuna chanjo iliyotengenezwa bado.

Wasomi wanasemaje?

n

Chanzo cha picha, Getty Images

Profesa Andy Pollard, mkurugenzi wa Taasisi ya Chanjo ya Oxford, hakuhusika katika utafiti huo, lakini anasema mbinu hii inatoa ushahidi wa kuvutia katika utafiti wa wanyama.

Amesema akili unde itakuwa muhimu kwa utafiti wa chanjo, kwani ina uwezo wa kutabiri jinsi mfumo wa kinga utakavyoitikia chanjo, na hivyo kuharakisha maendeleo na “kuokoa maisha.”

Profesa Marian Knight, Mwanasayansi katika Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa masuala ya Afya, anasema: “Mafanikio ya ajabu ya jaribio hili lililoundwa kwa akili unde, linaashiria hatua muhimu katika uwezo wetu wa kutoa ulinzi mpana na wa kudumu dhidi ya virusi.”

Lord Vallance, Waziri wa Sayansi wa Uingereza, amesema: “Haya ni mafanikio mengine ya kisayansi nchini Uingereza, huu ni mfano mzuri wa jinsi tunavyoweza kuchanganya utaalamu wetu wa utafiti na akili unde ili kutoa matibabu mapya.”

“Kwa majaribio ya awali kwa binadamu kutoa matokeo chanya, utafiti huu unaweza kuchangia kuharakisha usambazaji wa chanjo kwa manufaa ya watu duniani kote kwa muda mrefu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *