Serikali ya Marekani imesema itasitisha ufadhili wa miradi ya kupambana na Ukimwi Afrika Kusini ,hatua ambayo inahusishwa na tuhumu za Pretoria kushindwa kuwalinda raia wazungu nchini humo ,madai ambayo Afrika kusini imeyakanusha mara kadhaa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilionekana kuhusisha uamuzi huo na madai ya Afrika Kusini kushindwa kulinda jamii ya Waafrika walio wachache, madai ambayo serikali ya Afrika Kusini imekanusha mara kwa mara.

Wizara ya afya ya Afrika Kusini imesema kwamba ingawa haijafahamishwa kuhusu uamuzi huu, imekuwa ikifanya kazi kwa muda mrefu katika mpango wa kujitegemea.

Hadi mwaka wa 2025, Marekani ilikuwa ikiunga mkono juhudi za Afrika Kusini kukabiliana na virusi hivyo kwa ufadhili wa dolla Milioni 400 kwa mwaka kupitia Mfumo wa Dharura wa Rais.

Lakini tangu kuingia madarakani kwa Rais Donald Trump, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umezidi kuharibika. Zaidi ya Waafrika Kusini milioni nane wanaishi na Virusi vya Ukimwi , hii ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya nchi yoyote duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *