Rais William Ruto wa kenya, siku ya Jumanne anatarajiwa kutia Saini muswada wa fedha 2024, baada ya bunge la kitaifa wiki iliopita kuuidhinisha katika hatua ambayo imezua mjadala mpya wa kisiasa na kikatiba.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili, rais Ruto alithibitisha kuwa maandalizi ya sherehe za kusaini muswada huo yamekamilika huku akiwapongeza wabunge waliohakikisha muswada huo umepitishwa.

Musada huo wa fedha uliidhinishwa bungeni baada ya wabunge kupiga kura ya kuunga mkono hatua za ushuru na mapato zinazotarajiwa kufadhili vipaumbele kwenye bajeti ya serikali katika mwaka wa fedha ujao.

Hata hivyo, kupitishwa kwa bajeti hiyo kumezua ukosoaji kutoka kwa sehemu ya upinzani na baadhi ya viongozi wa chama cha ODM, wanaokosoa uhalali wa mchakato wa bunge ambao wanasema huenda haukufikia matakwa ya kikatiba.

Gavana wa Siaya James Orenge ni miongoni mwa viongozi wa ODM wanaokosoa mchakato huo, huku akimtaka rais Ruto kutotia Saini muswada huo kuwa sheria na badala yake kumtaka aurejeshe bungeni.

Licha ya ukosoaji huo, utawala wa kenya kwanza umeteta mswada huo wa fedha, ukisema unalenga kuiweka nchi katika hali nzuri kiuchumi pamoja na kuongeza ukusanyaji wa mapato.

Haya yanajiri wakati huu kukiwa na maandamano yanayopangwa kufanyika Juni 25 kuwakumbuka waathiriwa wa maandamano ya  2024 ya kupinga serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *