Massachusetts. Marekani. Kiungo wa England, Jude Bellingham amesema hakustahili kuwa mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa mech ya timu yake dhidi ya Ghana jana Jumanne, Juni 23, 2026.

Mara baada ya mchezo huo uliochezwa katika jimbo la Massachusetts, Bellingham alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi, tuzo ambayo nyota huyo wa England anaamini kwamba ilipaswa kwenda kwa mchezaji mmojawapo wa Ghana.

Bellingham ambaye ni kiungo mshambuliaji, amesema kuwa waliostahili kupata tuzo hiyo ni Ghana ambao walijilinda vizuri dhidi yao.

“Nilikuwa na nyakati kadhaa. Ilikuwa ngumu kuwa mchezoni. Namshukuru kila aliyenipigia kura lakini ilipaswa kwenda kwa wale waliojilinda vyema, hivyo pongezi kwao.

Nyota wa timu ya taifa ya England, Jude Bellingham wakati akizungmza kwa njia ya kuziba mdomo na mshambuliaji wa Ghana, Jordan Ayew. Picha na Mtandao

“Nadhani walikuja kucheza kwa ajili ya kutafuta sare kama ambavyo ilionekana na pongezi kwao kwa vile wamepata sare,” amesema Bellingham.

Katika mchezo huo, England ilionekana kuwa bora katika kumiliki mpira, kutengeneza nafasi na kulishambulia mara kwa mara lango la Ghana lakini haikufanikiwa kutikisa nyavu.

England ilipiga mashuti 19 huku Ghana ikifanya hivyo mara mbili tu. Pia England ilimaliza mchezo ikiwa na kona tisa lakini safu ya ulinzi ya Ghana ikiongozwa na kipa anayechezea Hearts of Oka ya kwao, Benhamin Asare ilikuwa makini kuondoa hatari hizo.

Baada ya sare hiyo, England sasa inahitaji sare aun ushindi wa aina yoyote katika mchezo wa mwisho dhidi ya Panama, Juni 28 ili iweze kujihakikishia kufuzu hatua ya 32 bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *