Mtandao wa Al Jazeera umeripoti uwepo mkubwa wa alama, nembo na bendera za Palestina katika mashindano ya Kombe la Dunia la Mpira wa Miguu 2026 yanayoendelea huko Marekani, Canada na Mexico.

Mtandao wa Al Jazeera umesema katika ripoti yake kwamba Kombe la Dunia la Mpira wa Miguu 2026 linashuhudia uwepo mkubwa wa alama na bendera za Palestina. Watazamaji na mashabiki wengi wanaonyesha hamu ya kupeperusha bendera za Palestina ndani na nje ya viwanja vya michezo, na mara kwa mara wanapaza sauti na  kaulimbiu za kulaani ukaliaji mabavi wa ardhi za Palestina unaofanywa na utawala haramu wa Usrael na kutaka uhuru pamoja na Palestina kuwa na mamlaka ya kujitawala.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wafuasi wa Palestina wanaounga mkono timu zinazoshiriki katika mashindano hayo wanaongoza kwa kiwango kikubwa shughuli za kuonyesha mshikamano na Palestina. Hali hii imesababisha maeneo yanayofanyika mechi za Kombe la Dunia kuwa jukwaa la kimataifa la kuonyesha uungwaji mkono wa wananchi kwa Palestina na kupinga sera za ukaliaji mabavu zinazotekelezwa na Israel.

Katika muktadha huo, video iliyochapishwa na shabiki mmoja wa Iran kwenye Instagram imeonyesha mwitikio mkubwa wa mashabiki kutoka mataifa mbalimbali yanayoshiriki katika Kombe la Dunia 2026. Mwitikio huo unaonekana wazi kuonyesha uungaji mkono wa umma kwa  haki za Palestina.

Video hiyo inajumuisha kura ya maoni ambayo mashabiki wanaombwa kwa hiari kuchagua kati ya bendera ya Palestina na bendera ya utawala wa Kizayuni unaokalia ardhi za Palestina. Matokeo yanaonyesha kwamba idadi kubwa sana ya majibu na maoni yaliyotolewa na mashabiki yalikuwa ya kuunga mkono bendera ya Palestina kama ishara ya mshikamano na wananchi wa Palestina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *