Uelewa mdogo wa sheria za usafirishaji wa bidhaa kutoka Tanzania kwenda China umetajwa kuwa moja ya vikwazo vikubwa vinavyowazuia wafanyabiashara wengi kunufaika na fursa zilizopo katika soko la China.

Balozi wa Tanzania nchini China, Suleiman Khaji Suleiman amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na China, ikiwemo biashara na utalii.

Amefafanua kuwa uimarishaji wa uelewa wa sheria na taratibu za biashara kati ya nchi hizo mbili unaweza kuongeza ushiriki wa wafanyabiashara wa Tanzania katika soko la kimataifa.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *