Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda ameiagiza Tume ya Ushindani (FCC) kuongeza matumizi ya teknolojia za kisasa katika kubaini na kufuatilia bidhaa bandia, hususan kupitia biashara za kidijitali na maeneo ya mipakani, ili kuimarisha mapambano dhidi ya bidhaa hizo nchini.

Mapunda ametoa maelekezo hayo katika kilele cha maadhimisho ya udhibiti wa bidhaa bandia yaliyoandaliwa na FCC, ambapo pia amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya tume hiyo, vyombo vya dola, mamlaka za forodha na taasisi nyingine za udhibiti ili kuwabaini na kuwachukulia hatua za haraka wanaojihusisha na uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa bidhaa bandia.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Khadija Ngasongwa, amesema zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa zinazoingia bandarini hukaguliwa kwa kutumia mifumo maalumu ya kutambua bidhaa bandia, hatua iliyoongeza ufanisi katika udhibiti na utekelezaji wa majukumu ya FCC.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *