Duru ya tano ya mazungumzo kati ya Israel na Lebanon, yaliyoratibiwa na Marekani na kutarajia kumalizika siku ya Alhamisi, Juni 25, sasa yataendelea leo Ijumaa, Juni 26, mjini Washington, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetangaza.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Nje imesema kwamba “majadiliano kati ya Israel na Lebanon bado yanaendelea” mjini Washington na yataendelea Ijumaa, Juni 26, “kwa lengo la kufikia makubaliano,” ingawa awali yalitarajiwa kukamilika siku ya Alhamisi. Hii inakuja huku shambulio la ndege zisizo na rubani za Israel dhidi ya gari moja kusini mwa Lebanon likiwaua watu watatu na kumjeruhi mmoja, kulingana na vyombo vya habari vya serikali, licha utulivu kuripotiwa kati ya Israel na Hezbollah. Hii inafikisha idadi ya vifo katika mashambulizi ya Israel tangu siku ya Jumanne hadi saba.

“Mazungumzo kati ya Israel na Lebanon bado yanaendelea tunapoendelea kuyawezesha.” Pande hizo mbili zitaanza tena mazungumzo kesho saa 3:00 asubuhi ili kuendelea na kazi yao kuelekea makubaliano,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ililiambia shirika la habari la AFP Alhamisi.

Hezbollah inayounga mkono Iran iliishutumu tena Israeli siku Alhamisi kwa “ukiukaji mkubwa” wa usitishaji mapigano baada ya shambulio la ndege zisizo na rubani kuwaua watu watatu. Jeshi la Israel lilidai kuwaua wapiganaji kutoka kundi hilo la Mashia.

Itifaki ya mkataba wa makubaliano kati ya Iran na Marekani yaliyosainiwa Juni 17 yanaeleza kukomeshwa kwa uhasama, ikiwa ni pamoja na Lebanon. Iran ilisisitiza kwamba suala hili lijumuishwe katika makubaliano ya itifaki ya mkataba wa makubaliano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *