Mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu nchini Tunisia, Sihem Bensedrine, amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela, kwa mashtaka ikiwemo kughushi sehemu ya ripoti ya mwisho ya tume ya mpito ya haki IVD iliochapishwa 2020, hata hivyo anapanga kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mwaka wa 2011, Tunisia iliibuka kutoka kwenye harakati za kuleta demokrasia maarufu kama Arab Spring Uprising kama ishara ya matumaini ya kidemokrasia katika eneo hilo baada ya miongo kadhaa ya utawala wa kimabavu, lakini sasa makundi ya haki za binadamu nchini humo yanaripoti kudorora kwa demokrasia chini ya rais Kais Saied.

Kulingana na Bensedrine, uamuzi huo hauhusishwi kivyovyote na haki bali unahusiana na utawala wa kidikteta unaotaka kufuta mafanikio ya tume hiyo ya haki na ukweli ambayo kipindi hicho alihudumu kama rais.

Ripoti ya mwisho ya tume hiyo ilitoa wito wa kuvunja mfumo wa ufisadi, ukandamizaji na a udikteta ndani ya taasisi za serikali.

Tume ya IVD iliundwa baada ya mapinduzi ya 2011 yaliomuondoa madarakani mtawala wa muda mrefu Zine El Abidine Ben Ali, ili kusikiliza ushuhuda kutoka kwa maelfu ya wahanga wake na wale wa mtangulizi wake Habib Bourguiba.

Bensedrine ameongeza kuwa amekuwa akilengwa na maafisa wanaoshikilia nchi mateka kwa lengo la kulipiza kisasi na kudhalilisha kazi waliofanya kama tume.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *