Katika taarifa yake iliyotolewa jioni ya tarehe 03 Oktoba 2025 majira ya jioni kwa saa za Marekani, na Msemaji wake Stéphane Dujarric imeeleza kuwa Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezihimiza pande zote kuchangamkia fursa hiyo ili kufikisha kikomo kwenye mzozo wa kikatili unaoendelea huko katika Ukanda wa Gaza.

“Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kuishukuru Qatar na Misri kwa juhudi zao muhimu za upatanishi.” Imesema taarifa hiyo na kuongeza kuwa “Guterres amerudia wito wake wa kudumu wa kusitishwa mara moja na kwa kudumu kwa mapigano, kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa mateka wote, na kupatikana bila vikwazo kwa misaada ya kibinadamu.”

Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa utaunga mkono juhudi zote zinazolenga kufanikisha malengo hayo ili kuzuia mateso zaidi kwa wananchi.

Vifaa vya matibabu vinatayarishwa kwa ajili ya kupelekwa katika ghala la WHO huko Gaza.

Vifaa vya matibabu vinatayarishwa kwa ajili ya kupelekwa katika ghala la WHO huko Gaza.

Fletcher: “Dirisha la fursa”

Mapema kabla ya kutolewa kwa tamko la Hamas, Mkuu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, alisema kuwa Umoja wa Mataifa iko tayari na inasubiri kuchukua hatua kupitia “dirisha la fursa” lililotolewa na mpango wa Marekani kuhusu Gaza.

Alieleza kuwa tani 170,000 za chakula, dawa, makazi na misaada mingine inayohitajika kwa dharura ziko tayari kuingizwa katika Ukanda wa Gaza kutoka maeneo mbalimbali ya kanda hiyo.

Hata hivyo, Fletcher alisema kuwa ni lazima vituo vya mpakani vinavyodhibitiwa na Israel vifunguliwe, kuwe na harakati salama kwa raia na wahudumu wa misaada, uingizaji wa bidhaa bila vizuizi, upatikanaji wa visa kwa wafanyakazi, kuwe na nafasi kwa mashirika ya misaada kufanya kazi, na sekta binafsi kufufuliwa.

Timu za misaada za Umoja wa Mataifa zinaonya kuwa hali kaskazini mwa Gaza inaendelea kuzorota kwa kasi huku Israel ikiendeleza mashambulizi ya kijeshi ili kudhibiti kabisa Jiji la Gaza, ambapo makumi ya maelfu ya raia wa Kipalestina hawana njia ya kutoroka.

“Operesheni za kijeshi na mashambulizi makali yanayolenga maeneo ya makazi na majengo yanaendelea kuongeza idadi ya vifo na kuharibu zaidi eneo hilo,” alisema Msemaji wa Katibu Mkuu, Stéphane Dujarric, katika mkutano wa kila siku na waandishi wa habari mjini New York, Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *