Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewahakikishia wananchi wakiwamo wageni kutoka nje ya nchi, usalama wa kutosha katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salam (Sabasaba) kwani ulinzi umeimarika huku akionya yeyote atakaye kwenda kinyume atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Chalamila, ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam, akizungumzia maandalizi ya maonesho hayo ambapo ufunguzi wa awali utafanyika kesho Jumapili, Juni 28, 2026 na ufunguzi rasmi Julai 3.
“Kutokana na ugeni mkubwa wa maonesho haya ya kimataifa, tumejipanga vyema kwa kiwango ambacho hakijawahi kuonekana, niwadhibitishie kuwa hakuna mtu yeyote atakaye hamasisha vurugu ukanda wowote wa Mkoa akabaki salama.
Ameyataja baadhi ya mataifa yaliyodhibitisha kushiriki katika maonyesho hayo ni China, Misri, Rwanda, Japani, Poland, Korea Kusini, Parestina, Sria, Falme za Kiarabu, Taiwan, Urus, Singapore, Msumbiji na Burundi, Ghana, Kenya, Uganda, Angola na Mengineyo.
Amesema maonesho hayo ni kielelezo cha fahari ya Utanzania na utamaduni wa Mtanzania na kwamba tutaendelea kuhamasisha wananchi wote kushiriki kufanya biashara na kulinda amani ya Taifa letu kwa kukataa vurugu.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni Bidhaa za Tanzania Kimatiafa zaidi, Sabasaba 2026 ni kubwa kuliko “

(Feed generated with FetchRSS)