Bruno GuimarĂ£es

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 2

Arsenal wanapanga kuongeza wachezaji watano zaidi dirisha hili la usajili, huku kinda wa Leicester City, Jeremy Monga (16), Bruno GuimarĂ£es wa Newcastle na Morgan Rodgers wa Aston Villa wakiwa miongoni mwa wanaowindwa. (Star, external)

Newcastle United bado hawajapokea ofa yoyote rasmi kwa ajili ya kiungo wao Bruno Guimaraes, licha ya taarifa zinazomhusisha na kuhamia Arsenal. (Chronicle)

Winga wa Ivory Coast Yan Diomande amechagua kujiunga na Paris St-Germain iwapo ataondoka RB Leipzig majira haya ya kiangazi, licha ya kuripotiwa kuwaniwa na Liverpool na Real Madrid. (Athletic)

Kiungo wa Liverpool, Curtis Jones, anawaniwa na Nottingham Forest, huku Liverpool wakimthaminisha kwa takribani pauni milioni 40. (Talksport)

Kiungo wa Manchester United, Mason Mount (27), amepewa nafasi ya kujiunga na AC Milan kwa ajili ya kuungana tena na kocha wake wa zamani Ruben Amorim. (MilanPress)

Hata hivyo, hadi sasa hakuna mawasiliano rasmi yaliyofanyika kati ya Manchester United na AC Milan kuhusu uhamisho huo. (Manchester Evening News)

a

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo wa Sunderland, Granit Xhaka, ameripotiwa kukubaliana masharti binafsi na Chelsea, huku akitaka kuhamia London na kufanya kazi tena na Xabi Alonso, ambaye aliwahi kuwa kocha wake akiwa Bayer Leverkusen. (Fabrizio Romano)

Chelsea wanafikiria kumsajili beki wa kushoto wa Rayo Vallecano, Pep Chavarria (28), kama mbadala wa Marc Cucurella, ambaye ameripotiwa kuhamia Real Madrid. (Marca)

Kiungo wa Monaco, Maghnes Akliouche, amewaambia Liverpool na Manchester United kuwa kipaumbele chake ni kujiunga na Paris St-Germain msimu huu wa kiangazi. (Teamtalk)

Aston Villa wako nyuma ya Leeds United katika mbio za kumsajili kipa wa Japan Zion Suzuki kutoka Parma. (Calciomercato)

Beki wa kulia wa Chelsea, Malo Gusto, ameripotiwa kukubali kujiunga na Manchester City, akitaka kuungana tena na kocha wake wa zamani Enzo Maresca. (Footmercato)

Juventus wamemuongeza kipa wa Aston Villa na Argentina, Emiliano Martinez (33), kwenye orodha yao ya wachezaji wanaowataka dirisha hili la usajili. (Tuttomercatoweb)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *