Kwa miezi kadhaa, matamshi dhidi ya wahamiaji yamekuwa yakiongezeka nchini Afrika Kusini, na hivyo kuwalaziu wahamiaji kadhaa kuondoka nchini humo wakati tarehe 30 Juni ikikaribia, tarehe ambayo wahamiaji wasio na vibali wametakiwa kuondoka nchini Afrika Kusini.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mwanzoni mwa mwezi Juni, wanaume wawili walitoa kauli ya mwisho kwa mkulima huyu wa Malawi, Kaunga Nyirenda, ambaye anaishi katika vitongoji vya Johannesburg: kuondoka mara moja au kufa.

“Waliniuliza unapanga kuondoka lini nchini tunataka kuiweka sawa nchi yetu, usipoondoka sasa utaondoka ukiwa ndani ya jeneza maana hatuhitaji mgeni yeyote baada ya Juni 30,” alisema.

Maneneo haya alioambiwa Nyirenda yanaonyesha kuongezeka kwa jumla kwa hisia za kupinga wahamiaji. Katika wiki za hivi karibuni, makundi ya waandamanaji na wanaojiita wanamgambo, ambao wanadai maandamano yao ni ya amani, wamefanya maandamano ambayo yameonekana kuibua mashambulizi makali dhidi ya raia wa kigeni, wasio kuwa na vibali au wale wanaoishi kisheria nchini humo. Wawili hao wanatuhumiwa kuiba kazi za Waafrika Kusini, kufanya uhalifu na kulemea huduma za umma.

Serikali ya Afrika Kusini imefutilia mbali kile kinachoitwa “makataa” yaliowekwa na makundi haya kwa wageni kuondoka nchini, huku hofu ya kuzuka kwa ghasia mwishoni mwa mwezi ikiongezeka.

Moja ya makundi haya, March & March, limetoa wito wa maandamano makubwa siku ya Jumanne ikiwa matakwa yake, ikiwa ni pamoja na “kufukuzwa mara moja na kwa wingi kwa wageni wote haramu kwa sasa katika eneo hilo”, hayatatekelezwa.

Kabla ya maandamano yaliyopangwa, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alionya kwamba serikali “haitavumilia jaribio lolote la kuhatarisha usalama wa taifa, iwe kwa maandamano au vinginevyo.”

Amelaani mara kwa mara mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni, akisema “hayawakilishi maoni ya raia wa Afrika Kusini wala sera ya serikali yetu.” Ramaphosa alisema vikosi vya usalama viko katika hali ya tahadhari kujibu machafuko yoyote.

Wahamiaji wanahofia usalama wao

Kutokana na mvutano unaozidi kuongezeka, polisi wa Afrika Kusini wamefungua uchunguzi kuhusu mauaji ya hivi karibuni ya raia kadhaa wa kigeni.

Polisi walisema raia wawili wa Msumbiji waliuawa wakati wa ghasia mwishoni mwa mwezi Mei huko Mossel Bay, mji wa pwani katika Rasi ya Magharibi, ambapo zaidi ya vibanda 50 katika eneo la vijijini vilichomwa moto. Msumbiji baadaye ilitangaza vifo vya raia wake watano katika kile ilichokiita “mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *