Umoja wa Ulaya (EU) umeamua kuweka vikwazo kadhaa vya visa kwa raia wa Somalia. Hawataweza tena kupata visa za kuingia mara nyingi za Schengen na muda wa kushughulikiwa kwa maombi yao ya visa utaongezwa kutoka siku 15 hadi 45. Pia hawatastahiki tena msamaha wa ada za pasipoti za kidiplomasia, wala kwa taratibu kadhaa zilizorahisishwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii, ambayo inakuja huku sera ya uhamiaji wa Ulaya ikizidi kuwa ngumu na kutokubaliana kuhusu kurejeshwa tena kwa wahamiaji wasio na vibali halali katika nchi zao za asili, ilizungumziwa sana na rais wa Somalia wakatiwa sherehe za maadhimisho ya miaka 66 ya uhuru wa Somalia.

Kujibu ukosoaji kutoka EU, ambayo inalaani ukosefu wa ushirikiano kutoka Mogadishu kuhusu kurejea kwa Wasomali waliofukuzwa kutoka eneo lake, Hassan Sheikh Mohamoud alibainisha kwamba nchi yake iko tayari kuwapokea raia wake. “Hatujawakataa raia wetu. […] Ikiwa ni Wasomali, tutawakubali,” alitangaza, akiongeza sharti moja.

Rais wa Somalia anasisitiza kwamba wale waliorudishwa nchini mwake lazima wawe raia wa Somalia, jambo ambalo anadai si mara zote huwa hivyo. Kulingana na rais wa Somalia, ingawa hawazungumzi lugha ya taifa ya Somalia, baadhi ya raia kutoka nchi zingine za Pembe ya Afrika wanajitambulisha kama Wasomali kwa matumaini ya kupata hifadhi barani Ulaya.

Nchi chache tayari zimelengwa na maamuzi kama hayo kutoka EU, kama vile Gambia, iliyochukuliwa vikwazo mwaka wa 2021, na Ethiopia, mwaka wa 2024. Hata hivyo, hatua zilizochukuliwa dhidi ya Banjul na Addis Ababa ziliondolewa mwez Mei mwaa huu, kufuatia ushirikiano ulioboreshwa na EU kuhusu kurejea na kurejeshwa kwa raia wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *