#MICHEZO: Kocha Mkuu wa Yanga, Ahamid Moallin, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa mwisho wa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania, mechi yenye uzito mkubwa katika kuamua hatima ya ubingwa wa msimu huu. Moallin amesema maandalizi ya timu yamekwenda vizuri na kwamba watayakamilisha katika mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo huo muhimu.

“Kwanza kabisa, maandalizi yetu ya mchezo wa kesho yamekwenda vizuri na InshaAllah leo jioni tunakwenda kukamilisha. Malengo yetu ni kushinda mechi ya kesho ili kutimiza malengo ya msimu mzima,” amesema Moallin, akisisitiza kuwa ushindi ndiyo kipaumbele cha timu yake katika pambano hilo la mwisho.

Yanga itaingia uwanjani ikiwa na dhamira ya kuvuna pointi tatu muhimu zitakazoiweka katika nafasi nzuri ya kutimiza ndoto ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Mashabiki wa soka nchini wanasubiri kwa hamu mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku matokeo yake yakitarajiwa kuamua bingwa wa msimu wa 2025/26.

Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *