f

Chanzo cha picha, Getty Images

Spika wa Bunge la Iran na mpatanishi mkuu wa nchi hiyo, Mohammad Baqer Qalibaf, ametoa wito kwa Wairani kushiriki kwa wingi katika mazishi ya Kiongozi Mkuu wa zamani wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, akisema ushiriki huo utakuwa sehemu ya kulipiza kisasi kwa kifo chake.

Katika taarifa yake Alhamisi, Qalibaf alisema, “Ninawaomba wananchi wote wa Iran kuandika ukurasa wa kihistoria wa Iran ya Kiislamu kwa kushiriki katika mazishi ya Khamenei.”

Aliongeza kuwa, “Wito wa taifa wa kulipiza kisasi lazima usikike duniani kote.”

Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran limesema litachukua hatua za kulipiza kisasi kwa kifo cha Kiongozi Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Ayatollah Ali Khamenei.

Katika taarifa iliyotiwa saini na Katibu wa Baraza hilo, Mohammad Baqer Zolqadr, Iran imesema “kisasi kwa damu ya Ayatollah Ali Khamenei kitachukuliwa dhidi ya waliomuua.”

Khamenei aliuawa Februari 28 wakati wa siku ya kwanza ya mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Wakati huo huo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan ametangaza kuwa Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, atashiriki katika shughuli za mazishi ya Khamenei zitakazoanza Jumamosi mjini Tehran.

Kwa mujibu wa BBC Persian, shughuli za mazishi ya Khamenei zitafanyika kati ya Julai 4 na 8 katika miji ya Tehran, Qom na Mashhad, huku mikutano ya maombolezo pia ikipangwa kufanyika katika miji ya Baghdad, Kazmin, Karbala na Najaf nchini Iraq.

Unaweza kusoma;

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *