
Wizara ya Usalama ya Iran imeapa kulipiza kisasi damu ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, ikisisitiza kuwa mioyo iliyojeruhiwa ya wananchi wa Iran na wapenda uhuru duniani kote haitapata faraja yoyote isipokuwa kwa kulipiza kisasi dhidi ya wahusika.
Katika taarifa yake jana Jumamosi, wizara hiyo imeeleza kuwa taifa la Iran limekuwa katika maombolezo kwa zaidi ya miezi minne kufuatia kuuawa shahidi kiongozi wao.
Taarifa ya Wizara ya Usalama ya Iran imebainisha kuwa: Adui Marekani na Mzayuni wenye kiu ya damu walitenda jinaikubwa zaidi na njama ya kigaidi katika historia ya sasa kupitia janga hili kubwa.
Nyoyo zilizojeruhiwa za watu shupavu wa Iran na wapenda uhuru kote duniani hazitapata nafuu wala faraja yoyote isipokuwa kwa kulipiza kisasi dhidi ya wahusika wa uhalifu huu,” imeeleza taraifa ya Wizara yaUsalama ya Iran na kuongeza kuwa: “kulingana na ahadi ya Mwenyezi Mungu, kisasi na adhabu zitatimia.”
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa: Maafisa wa Wizara ya Usalama kwa lengo la kumuenzi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu shahidi Ayatullah Khamenei na mashahidi wengine wa familia yake wanatoa wito kwa taifa la Iran linalowapenda mashahidi kushiriki katika marasimu hayo makubwa na ya kihistoria ya kumuaga Imam wao aliyeuawa shahidi.
Kwa mara nyingine tena wamethibitish ahadi yao kwa Imam shahidi na kwa wananchi waIran ya kulipiza kisasi damu ya Ayatullah Seyyed Ali Khamenei aliyeuawa shahidi na mashahidi wengine wa mashambulizi mawili ya hivi karibuni ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.