Maafisa kutoka harakati ya muqawama wamekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi, na kuwasilisha salamu za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika mashambulizi ya kigaidi a Marekani na Israel dhidi ya Iran Februari 28 mwaka huu.

Mazungumzo hayo yalifanyika jana Jumamosi, pambezoni mwa shughuli za mazishi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi katika hujuma ya kikatli ya Marekani na utawala haramu wa Israel , mazishi ambayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na waombolezaji kati ya milioni 15 na 20.

Katika mauzngumzo hayo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Khalil Hamdan aliyewakilisha Harakati ya Amal ya Lebanon na Spika wa Bunge la nchi hiyo Nabih Berri, alifikisha ujumbe wa rambirambi kwa wananchi na serikali ya Iran.

Kwa upande wake, Araghchi amepongeza msimamo thabiti na imara wa wananchi wa Lebanon katika kukabiliana na vitisho na uchokozi wa utawala wa Israel.

Khalid Hamdan pia amesema kuwa anathamini msimamo imara wa Tehran katika kuunga mkono mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya Lebanon; na kusisitiza ulazima wa kusitishwa mashambulizi ya Israel dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Katika mkutano mwingine, Mohammad Fneish, ambaye alimwakilisha Sheikh Naim Qassem Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Lebanon Hizbullah alifanya mazungumzo na mwanadiplomasia mkuu wa Iran Sayyid Abbas Araghchi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Tehran inafuatilia kwa dhati kuhitimishwa vita dhidi ya Lebanon na kukomeshwa uvamizi wa Israel nchini humo kwa mujibu wa Kipengele cha 1 cha Mkataba wa Makubaliano (MoU) yaliyofikiwa kati ya Tehran na Washington.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *