Ripoti ya hivi karibuni kutoka kwa Kundi la Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inaangazia kuongezeka kwa mapigano karibu na Minembwe, katika nyanda za juu za mkoa wa Kivu Kusini, pamoja na kuzorota kwa hali ya kibinadamu kwa raia, haswa jamii ya Banyamulenge.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti hii, iliyowasilishwa Mei 8, 2026, kwa Kamati ya Vikwazo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wataalam wanaonyesha kwamba mwishoni mwa mwezi Januari 2026, Vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC), vinavyoungwa mkono na kundi la Wazalendo, vikosi vya jeshi la Burundi (FDNB), na makampuni ya kijeshi ya kibinafsi, vilianzisha shambulio kutoka Uvira kuelekea Minembwe dhidi ya kundi la waasi la MRDP/Twirwaneho na AFC/M23.

Vita vya kudhibiti Minembwe

“Mwishoni mwa mwezi Januari 2026, FARDC, kwa usaidizi wa Wazalendo, FDNB, na makampuni ya kijeshi ya kibinafsi, walianzisha mashambulizi kutoka Uvira kuelekea Minembwe dhidi ya MRDP/Twirwaneho na AFC/M23, huku kundi la AFC/M23 likiwa limetuma vikosi vya ziada kwa MRDP/Twirwaneho mnamo mwezi Agosti 2025 na Februari 2026. Inakadiriwa kuwa MRDP/Twirwaneho ilikuwa na wapiganaji kati ya 2,500 na 3,000, chini ya amri ya Charles Sematama,” kunlingana na ripoti ya Kundi la Wataalamu.

Kulingana na ripoti hiyo, uwepo wa jeshi la Rwanda (RDF) katika Nyanda za Juu ulipunguzwa kwa idadi wanajeshi waliowekwa kwa msingi wa dharura katika ngazi ya sehemu, pamoja na usaidizi wa anga, labda kutokana na kuwa ufikiaji wa eneo hilo ni mgumu. Kulingana na hati hiyo, wapiganaji wa MRDP/Twirwaneho na AFC/M23 walikusanyika tena karibu na maeneo ya raia kutoka jamii ya Banyamulenge, haswa Minembwe, Mikenge, na Muranvia.

Kwa wiki kadhaa, ripoti ya Kundi la Wataalamu la Umoja wa Mataifa inaongeza, FARDC ilikata njia za usambazaji kwenda Minembwe. Mnamo Machi 31, walianzisha shambulio kubwa katika mji huo baada ya kupata maendeleo endelevu katika Nyanda za Juu.

“Kwa kujibu, jehi la Rwanda (RDF) ilitoa msaada kwa MRDP/Twirwaneho na AFC/M23 kwa kufanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na kutoa usambazaji wa anga. Mashambulizi yaliyofanywa kati ya mapema na katikati ya mwezi Aprili yalilazimisha FARDC kujiondoa kutoka ngome muhimu, ikiwa ni pamoja na Muranvia, hali ambayo ilisitisha kwa muda kusonga mbele kwao,” ripoti inaelezea.

Raia wa Banyamulenge wakwama Minembwe

Kulingana na ripoti hiyo, idadi ya watu kutoka jamii ya Banyamulenge, walio ndani na karibu na Minembwe, wamekwama kutokana na mapigano yanayoendelea. Tangu katikati ya mwaka 2025, eneo hilo limezingirwa na FARDC (Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) na vikosi washirika, na hivyo kuzuia utoaji wa vifaa muhimu na misaada ya kibinadamu.

“Tangu Februari 2026, njia pekee inayowezekana ya kufikia imekuwa kwa njia ya anga. Njia zote za mawasiliano zimekatwa, na kuzidisha hali ya kibinadamu kuwa ngumu. Hata hivyo, MRDP/Twirwaneho imewazuia raia kuondoka Minembwe kwa hofu ya kuhama na uvujaji wa taarifa, hasa kupitia kulazimishwa na vitisho vya vurugu.” Kama ilivyoripotiwa hapo awali, wavulana wote wenye umri wa miaka 10 hadi 12 na wanaume wote wenye uwezo walilazimishwa kujiunga na Twirwaneho, kitendo ambacho ni ukiukaji wa marufuku dhidi ya kuajiri kwa lazima na kuajiri na kuwatumia watoto katika vita,” ripoti ya Jopo la Wataalamu la Umoja wa Mataifa inabanisha.

Hata hivyo, ripoti ya Jopo la Wataalamu la Umoja wa Mataifa inabainisha kwamba watu kutoka jamii ya Banyamulenge walishutumu pande zote mbili kwa kuwakwamisha raia katika eneo la mapigano, wakiitaka FARDC kuondoa vizuizi na kuanzisha ukanda wa kibinadamu, na kwa MRDP/Twirwaneho na AFC/M23 kuwaruhusu raia kuondoka katika eneo hilo salama.

“Tabia zilizoelezwa zinaibua wasiwasi mkubwa chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu, haswa kuhusu marufuku dhidi ya kuwatumia raia kama ngao za binadamu kulinda malengo ya kijeshi,” ripoti ya Jopo la Wataalamu la Umoja wa Mataifa inasema.

Kulingana na ripoti hiyo, viongozi wa MRDP/Twirwaneho na AFC/M23 walidai kwamba FARDC na FDNB walikuwa wamefanya kampeni ya kuwaangamiza, na iliyolenga watu kutoka jamii ya Banyamulenge, haswa kupitia mashambulizi anga katika maeneo yenye watu wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *