
Nchini Burkina Faso, wanajeshi wasiopungua hamsini na wale wanaojitolea kwa Ulinzi wa Nchi (VDP) waliuawa Jumamosi, Julai 4, katika mashambulizi mabaya yaliyofanywa na JNIM (kundi linalohusishwa na Al Qaeda).
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mashambulizi haya yalilenga maeneo kadhaa nchini: kaskazini, kaskazini magharibi, na kusini magharibi. Kambi kadhaa ziliporwa na silaha zilichukuliwa na wanajihadi.
Hadi sasa, hakujakuwa na majibu kutoka kwa mamlaka, lakini JNIM imedai kuhusika na mashambulizi haya, ambayo picha zake zinasambaa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Shambulio hilo lilianza Jumamosi asubuhi saa 11:00 alfajiri. Wapiganaji wa JNIM walivamia kambi ya kijeshi huko Di, katika jimbo la Sourou kaskazini magharibi mwa nchi. Baada ya mapigano makali, walifanikiwa kuingia katika kambi hiyo kabla ya kuondoka. Wakati wa shambulio hili, kulingana na chanzo chetu, angalau wanajeshi 23 na wanachama 11 wa VDP waliuawa.
Kwa upande wake, JNIM inadai katika video kuwa iliona miili 22 ya wanajeshi wa Burkina Faso na wanachama wa VDP kabla ya kujiondoa kutoka mji wa Di. Pia inadai kuhusika na mashambulizi mengine mawili katika sehemu za kusini magharibi na magharibi mwa kati mwa nchi, huko Dalan na Tiéré. Angalau wanajeshi 18 waliuawa katika mashambulizi haya. Vyanzo vingine kadhaa vinathibitisha uharibifu mkubwa wa vifaa katika maeneo haya mawili.
Siku hiyo hiyo, Jumamosi iliyopita, wanajihadi walishambulia miji ya Thiou na Séguénéga kaskazini mwa nchi. Hakuna vifo vilivyoripotiwa kufikia sasa, lakini magari mengi ya raia yalichomwa moto, kulingana na mashahidi.
Hadi sasa, hakuna jibu kutoka kwa jeshi au serikali ya Burkina Faso kuhusu mashambulizi haya.