Serikali imewaomba wadau wa maendeleo kuendelea kuunga mkono utekelezaji wa sera ya elimu bila ada ili kusaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, ikiwemo kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madawati.
Takwimu za Serikali zinaonyesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita inahitaji jumla ya madawati 93,740, huku yaliyopo yakiwa 50,489 pekee. Hali hiyo imeacha upungufu wa madawati 43,251, sawa na asilimia 46 ya mahitaji halisi.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)