Mkutano wa viongozi wa muungano wa kujihami wa NATO umeanza mjini Ankara, Uturuki, ukijadili masuala mbalimbali yanayohusu usalama wa Ulaya, vita vinavyoendelea nchini Ukraine pamoja na mwelekeo wa ushirikiano wa kijeshi kati ya Marekani na washirika wake wa Ulaya.
Katibu Mkuu wa NATO, Mark Rutte amesema Ulaya kwa sasa ni mshirika muhimu zaidi wa Marekani kuliko ilivyokuwa miaka mitano iliyopita, huku akisisitiza umuhimu wa mataifa ya Ulaya kuongeza uwezo wao wa kujilinda na kupunguza utegemezi wa kijeshi kwa Marekani.
Amesema ushirikiano wa karibu kati ya Marekani na washirika wake wa Ulaya utaendelea kuwa nguzo muhimu katika kukabiliana na changamoto za usalama zinazolikabili eneo hilo na dunia kwa ujumla.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)