Nchini DRC, baraza la Seneti siku ya Jumanne ilikubali rasimu ya sheria ya bajeti ya ziada ya 2026 iliyowasilishwa na Naibu Waziri Mkuu anayesimamia Bajeti, Adolphe Muzito.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ingawa bajeti ya serikali imepunguzwa, serikali inasisitiza kwamba ulinzi na usalama vinasalia kuwa miongoni mwa vipaumbele vyake vikuu.

Bajeti iliyorekebishwa imepunguzwa hadi Dola bilioni 21.9, upungufu wa asilimia 7.4 ikilinganishwa na sheria ya awali ya bajeti, hasa kutokana na kupungua kwa rasilimali za nje.

Licha ya kupunguzwa huku, Naibu Waziri Mkuu wa Bajeti na Fedha, Adolphe Muzito, aliwaambia maseneta kwamba sera kuu zinazofadhiliwa na bajeti hii ya ziada zinalenga matumizi ya ulinzi na usalama. Alitaja nyumba za polisi, usafiri, na kambi za kijeshi kama vipaumbele.

Ripoti kutoka kwa Kamati ya Masuala ya Uchumi ya Bunge la Kitaifa inaunga mkono mtazamo huu. Inaonyesha kwamba matumizi ya usalama yameongezwa kwa asilimia 31.4 ili kuimarisha usaidizi kwa vikosi vya ulinzi na usalama.

Wakati wa kikao chake, Adolphe Muzito, kwa upande wake, alitaja ongezeko la asilimia 34.4, ambalo alilihalalisha kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama mashariki mwa nchi.

Katika Seneti, maseneta kadhaa walitaka kupita zaidi ya takwimu hizi. Mmoja wao alisema kwamba, licha ya juhudi hizi kubwa za kifedha kwa ajili ya ulinzi wa taifa, serikali haijapendekeza utaratibu wowote ulioimarishwa wa usimamizi wa bunge wa matumizi haya ya usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *